The premier destination for premium products

Utumaji na Urejeshaji

Bei Chee ndio mmiliki kamili wa bidhaa zote mpaka hapo malipo kamili yatakapopokelewa.

Inawezekana kufuta oda yako kama bado haijatumwa. Wasiliana nasi na tutakusaidia. Kama oda yako tayari imetumwa, utalazimika kurudisha bidhaa ili kurejeshewa fedha zako. Gharama za usafirishaji hazitorudishwa. Haiwezekani kubadili oda yako mara baada ya kuiwasilisha. Hii inajumuisha kubadili saizi au rangi ya bidhaa yako, kuondoa bidhaa, kubadili anwani ya kupokea oda au njia ya malipo.

Bidhaa zote zinatumwa na timu yetu kutoka Dar es Salaam. Oda yako itatumwa ndani ya saa 24 kama inapokelewa Dar es Salaam. Nje ya Dar es Salam tutafanya juhudi kukufikishia ndani ya siku 7 za kazi.

 

Mida ya kawaida ya kukufikishia oda yako baada ya mzigo kutumwa ni

 • masaa 24 ndani ya Dar es Salaam
 • siku 7 kwa mikoani
 • Kama hakutakuwa na mtu yoyote kwenye anwani ya kupokea mzigo pindi unapofikishwa, tutaacha ujumbe na kuondoka na mzigo. Jitahada nyingine za kukufikishia mzigo zitafanyika siku itakayofuta. Tutajitahidi kukufikishia mzigo mara mbili. Kama itashindikana kupokea mzigo, utarudishwa kwetu.

  Unaweza pokea mzigo wako kwenye anwani yako ya kazini kama hii ni njia rahisi zaidi kwako. Hii ijumuishwe tu kwenye anwani yako ya kupokelea mzigo.

  Gharama za usafirishaji zinategemeana na anwani ya kupokelea mzigo.

   

  Gharama za usafirishaji ni kiasi gani?

  Tunasafirisha nchi nzima ya Tanzania, na gharama za usafirishaji zinategemea na anwani yako ya kupokelea mzigo na kiasi cha manunuzi yako. Tafuta eneo lako ya kupokelea na gharama za usafirishaji hapo chini – pamoja na kiwango cha usafirishaji wa bure.

  Dar es Salaam

  Gharama za usafirishaji: Bure

  Usafirishaji wa bure: Kwa bidhaa zenye thamani ya zaidi ya Tshs. 100,000 (chin ya Tshs. 100,000 utachajiwa Tshs. 5,000)

  Maeneo mengine Tanzania

  Gharma za usafirishaji: Tshs. 25,000

  Usafirishaji wa bure: Kwa bidhaa zenye thamani ya zaidi ya Tshs. 1,000,000

  Sera ya kurudisha bidhaa

  Bidhaa zote zinazouzwa chini ya Bei Chee, chini ya vigezo husika, zinaweza kurudishwa ndani ya siku 7 kutokea siku oda ilipopokelewa. Unaweza kututumia WhatsApp au barua pepe kuomba kurudisha bidhaa kwa kuweka nambari yako ya oda kwenye sehemu ya somo pamoja na neno – Rudisha mf. Rudisha Oda #0134962 na kisha tuma ujumbe ukielezea taarifa nyingine zote kwenda WhatsApp namba 0762 493 434 au barua pepe [email protected]

  Kisha itafuata uhitaji kwa taratibu sahihi ambapo taarifa nyingine zitathibitishwa na upande wa msimamizi na kuthibitishwa kupitia barua pepe/ simu kama ifuatavyo:

  • Uthibitisho wa manunuzi (namba ya oda, invoice nk.)
  • Sababu ya kurudisha lazima iwe sahihi na sifa za kurudisha lazima ziwezimekdhi (tazama jedwali hapo chini)
  • Njia ya kurudisha
  • Njia ya kurudishiwa fedha utakayopendelea na taarifa za muhimu zinazohusiana (namba ya akaunti, nk)
  • Fomu ya kurudisha irudishwe na bidhaa

   

  Pindi itatokea bidhaa imeharibika kutokana na njia yetu ya usafirishaji, tafadhali wasiliana na huduma kwa wateja masaa 24 kwa malalamiko. Tutaanda njia ya kuja kuchukua bidhaa husika ndani ya masaa 48 baada ya kuwasilisha maombi ya kurudisha.

  Zingatia, kuja kuchukua tutafanya jitihada mara 2.

  Aidha, baada ya jitihada hizo 2 kushindikana, tutalazimika kufuta taratibu za urudishaji na hutoweza kurudisha bidhaa husika kwetu tena.

  Baada ya bidhaa yako kupokelewa tutafanya uchunguzi wa ubora kwanza.

  Kama uchunguzi wa ubora ukiridhisha na kufanikiwa, tutarejesha fedha zako kwa njia uliyochagua. Hii itafanyika ndani ya siku 10 kwanzia siku maombi yako ya kurudisha yalipopokelewa. Zingtia, kama uchunguzi wa ubora hautafanikiwa, hautorudishiwa fedha zako na bidhaa yako utarudishiwa.

  All search results