The premier destination for premium products

Faragha

Sera ya Faragha

Taarifa zote unazotoa ni kwa lengo la kuboresha huduma zetu za kukuhudumia wewe kwa namna ya kipekee zaidi ili ufurahie manunuzi unayofanya. Taarifa zote zinatunzwa kwa siri na ni binafsi. Taarifa zako binafsi hazitapewa watu wengine, kusambazwa ama kuboreshwa kwa namna yoyote bila idini yako.

Kama ukiweka oda kwetu, tutahitaji taarifa zako binafsi. Ni muhimu utupatie taarifa zako za mawasiliano (kama vile jina, barua pepe na anwani) na taarifa za kifedha (kama vile namba za kadi za benki – credit card number, tarehe ya kuisha muda, na tarakimu tatu za kiusalama). Tunatumia taarifa hizi kwa lengo la kukamilisha malipo na oda yako. Tukipata tatizo katika kukamilisha oda, tutatumia taarifa zako za mawasiliano. Namba yako ya simu inahitajika kwa lengo la kukufikishia oda yako pindi tutakapo hitaji kuwasiliana nawe kuhusu sehemu ya kupokea oda yako.

Tunatumia tovuti nyingine kama Google Analytics kutoka Google kutusaidia kufahamu sehemu ambazo wageni wetu wanatembelea pindi wawapo kwenye tovuti yetu. Tunaidhini ya kuboresha sera hii ya faragha wakati wowote, hivyo tunaomba uipitie mara kwa mara. Kama tukifanya mabadiliko makubwa ya sera hii, tutakujulisha hapa na kwa notisi kwenye tovuti kiujumla.

Sera hii imeboreshwa kwa mara ya mwisho Juni 1 2017.

Matumizi ya Cookies

Cookies ni baadhi ya taarifa ambazo tovuti inahamisha kwenda kwenye hard disk ya kompyuta yako kwaajili ya kutunza kumbukumbu. Cookies zinaweza fanya tovuti iwe rahisi zaidi kutumia kulingana na unavyopendelea zaidi. Matumizi ya cookies yapo kwenye tovuti zote kubwa kwa lengo la kuboresha huduma kwa wateja kulingana na mahitaji yao. Ni sera yetu kutumia cookies kwa sababu zifuatazo tu:

  • Kukutambua wewe
  • Kuoanisha mahitaji yako na tovuti yetu
  • Kuboresha matumizi ya tovuti

Browsers nyingi zimewezeshwa kukubali matumizi ya cookies. Kama unapendelea, unaweza kuzuia browser yako ikatae cookies. Aidha, hutoweza kufurahia matumizi bora zaidi ya tovuti yetu.

Tunatumia teknolojia ya kufuatilia ili kuweza kuelewa zaidi mienendo na matumizi ya watu kwenye tovuti. Aidha, taarifa zote zinazokusanywa na teknolojia hii haziwezi kutambua taarifa binafsi za mtumiaji.

Disclaimer

Bei Chee imejikita, kwa jitihada zote, kukupatia taarifa sahihi na za wakati kwenye tovuti hii. Pamoja na hilo, mara chache kunaweza kutokea mabadiliko ya bei, bidhaa kuisha na matatizo mengine yasiyokusudiwa kwenye tovuti yetu. Tunahaki ya kutowajibika kwa matatizo hayo au mabadiliko na Bei Chee, wafanyakazi wake au wawakilishi wa Bei Chee hawatawajibika kwa matatizo yoyote yatokanayo na matumizi ya tovuti hii au bidhaa zilizouzwa hapa.

Sheria Inayotumika

Hivi vigezo na masharti vitatafsiriwa na kusimamiwa kulingana na sheria na taratibu zilizopo za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kila upande unakubali kuwajibika kulingana na mamlaka ya mahakama zilizopo Tanzania na kuacha vikwazo vyoyote kulingana na eneo.

All search results