The premier destination for premium products

Maswali

Kiujumla

Napaswa kufanya nini baada ya kuingia kwenye akaunti yangu?

Pindi umekamilisha uchaguzi wa bidhaa unayopenda kuinunua, fuata hatua zifuatazo:

 • Bofya kitufe chekundu cha “NUNUA SASA” kwenye bidhaa uliyochagua na kisha endelea
 • Tafadhali hakikisha unajaza taarifa zote muhimu kama vile jina, namba ya simu, barua pepe nk. Pia, waweze kuturahisishia zaidi kwa kujaza taarifa zaidi kwenye ‘Dondoo za oda’ ili tuweze kukufikishia oda kwa haraka zaidi
 • Sasa unaweza chagua jinsi ya kukamilisha malipo yaani kupitia PesaPal, Benki, au kwa njia ya simu pindi oda yako itakapokufikia.
 • Hatimaye, bofya WEKA ODA
 • Utapokea uthibitisho wa oda yako uliyoweka pamoja na namba ya kipekee ya oda (itunze!). Pia utapokea ujumbe wa simu pamoja na barua pepe kuthibitisha.

Ukipata changamoto yoyote wakati wa kuweka oda yako kupitia Bei Chee, tafadhali wasiliana nasi kupitia 0762 493 434 au WhatsApp kupitia namba hiyo hiyo.

Kwanini nifanye manunuzi kupitia Bei Chee?

 • Pata Bei Nafuu, Ndio…. Bei Nafuu! Usituamini tu, tulinganishe na wengine
 • Usafirishaji wa oda bila usumbufu. Pokea oda yako ndani ya masaa 2 Dar es Salaam*, hakuna trafik tena, foleni wala kusubiri bila sababu
 • Pokea bidhaa zako zote ukiwa umepumzika nyumbani bure. Ndio, BURE kuletewa bidhaa zako nyumbani*
 • Biashara yetu imejengwa kwenye misingi ya kuwahudumia wateja wetu kwa ubora wa hali ya juu. Mawakala wetu wa huduma kwa wateja wapo tayari kukuhudumia kwanzia saa 2 asubuhi mpaka saa 2 usiku.
 • Tunayo sera nzuri ya kurudisha bidhaa na fedha zako hivyo waweza pumzika bila wasiwasi baada ya kufanya manunuzi
 • Mwisho, lakini si kwa umuhimu, bidhaa zetu ni 100% halisi! Tunakuhakikishia bidhaa zetu ni za ubora wa hali ya juu zikiambatana na warantii pamoja na bidhaa zote hufanyiwa checkup ya ubora na uhalisia wa bidhaa

Nawezaje kujisajili kwenye tovuti yenu?

Kujisajili, tafadhali bofya kitufe cha jiunge kilichopo upande wa juu kulia kwenye ukurasa wa mwanzo wa Bei Chee. Utapelekwa kwenye ukurasa utakaokupa chaguzi mbalimbali ikiwemo furksa ya kuingia ndani kama tayari una akaunti au kujisajili kama mteja mpya kwa kuweka tu barua pepe yako. Utapokea jina la kutumia na neon siri kupitia barua pepe.

Naweza fanya nini baada ya kuingia Bei Chee?

Kujisajili kunakupa furksa na faida kadhaa wa kadhaa

 • Kuona hatua halisi ya oda yako
 • Kuona hatua za usafirishaji
 • Kufuta oda
 • Kuona kumbukumbu za nyuma za manunuzi yako
 • Ofa na vocha za punguzo mbalimbali

Naweza kuuuza bidhaa zangu kwenye tovuti yenu?

Kwa sasa hatuuzi bidhaa kutoka maduka mengine. Tumeondoa watu wa kati ili kuwapa wateja wetu bei nafuu na bidhaa bora.

Sioni bidhaa ninayoitafuta?

Unaweza kututumia ujumbe kupitia WhatsApp au barua pepe [email protected] ikiwa na kichwa cha habari “Tafuta Jina la bidhaa”. Unaweza wasiliana nasi pia kupitia 0762 493 434 au WhatsApp na tujulishe kuhusu bidhaa unayoipendelea. Pamoja na hilo, tuna bidhaa nyingine nyingi zinazoweza kuwa zinafanana na unayoitafuta, tunaweza kukusaidia kuchagua.

Nitegemee nini kwenye sehemu ya ‘Bidhaa Mpya’

Bidhaa Mpya ni sehemu yetu ya kuonesha bidhaa ambazo ni mpya kuzinduliwa sokoni au zinazokaribia kuzinduliwa. Tunakuletea dondoo za bidhaa hizo lakini pia tunakupa furksa za kuweka booking kabla ya uzinduzi.

Bidhaa za 'Dili Za Ajabu' ni bidhaa gani?

Bidhaa za ‘Dili Za Ajabu’ ni zile ambazo zina sifa za kipekee kwenye tovuti yetu. Bei Chee inachukua hatua za kipekee katika manunuzi ya bidhaa hizi na kuzileta kwa watu wa nyumbani Tanzania.

Bidhaa za 'Dili Za Ajabu' ni bidhaa gani?

‘Dili Za Ajabu’ inaweza kuwa muungano wa bidhaa 2 au 3 kwa bei ya punguzi. Inaweza pia kuwa zawadi ya bure pindi unaponunua bidhaa flani. Bei zilizokatwa kwa upande mwingine ni bidhaa ambazo zipo kwenye punguzo nk.

Utumaji na Urejeshaji

Mnaweza kupeleka oda nje ya Tanzania?

Kwa sasa hapana. Tupo kwenye lengo la kuwa duka la kwenye mtandao linaloaminika zaidi Tanzania.

Nitegemee lini kupokea bidhaa yangu baada ya kuweka oda?

Bidhaa zote zinatumwa na timu yetu kutoka kwenye ofisi zetu zilizopo Dar es Salaam. Oda yako hutumwa ndani ya saa 2 kama oda yako itapokelewa Dar es Salaam na kuwekwa kabla ya saa 8 mchana. Nje ya Dar es Salaam, tutajitahidi kukufikishia oda yako ndani ya siku 7 za kazi. Pindi tu oda imewekwa, tutathibitisha hali ya kupokea bidhaa yajo kupitia ujumbe wa simu na barua pepe.

Usafirishaji utafanyikaje?

Usafirishaji huzingatia taratibu sahihi za kibiashara bidhaa zako zitafungwa vema. Tafadhali usipokee bidhaa kama seal imechezewa.

Naweza kufuata bidhaa yangu badala ya kusubiri itumwe kupitia mtandao?

Ndio, inawezekana. Tembelea ofisi yetu Msasani Tower, Kimweri Avenue, Msasani, Dar es Salaam. Mida yetu ya kazi ni Jumatatu hadi Ijumaa saa 2 asubuhi hadi saa 11 jioni.

Gharama zenu za usafirishaji zipoje?

Kwa manunuzi yote ya zaidi ya Tshs. 100,000 usafirishaji ni bure ndani ya Dar es Salaam mjini.

Inakuaje kama nikiwa sipo nyumbani wakati bidhaa ikiletwa?

Kabla ya kuleta bidhaa yako, mwakilishi wetu mmoja atakupigia simu ambayo utakuwa umetupatia awali wakati wa kuweka oda yako ili kuhakikisha kama utakuwepo muda ambao anataka kukuletea bidhaa yako.

Naweza letewa oda yangu ofisini?

Ndio, unahitaji tu kuweka anwani unayopendelea kupokelea oda yako kwenye sehemu ya kupokelea

Sijapokea oda yangu bado, naweza kufanyaje?

Unaweza ifuatilia oda yako kupitia mtandao au wasiliana na huduma kwa wateja.

Malipo

Njia gani za malipo naweza tumia?

Bei Chee inakubali njia mbili pekee za malipo:

 1. Lipia mzigo ukifika

Hii ina maana unalipia bidhaa zako wakati wa kuzipokea. Unaweza kukamilisha malipo kwa njia ya miamala ya simu baada ya kukagua bidhaa.

Hii ni kwa wateja wa Dar es Salaam pekee.

 1. Malipo kupitia mtandao

Hii ina maana unafanya malipo kabla bidhaa haijakufikia (advance payment) kwa kukamilisha malipo yako mtandaoni.

 

Malipo kupitia mtandao yafanyike ndani ya masaa 12, tofauti na hapo oda hufutika yenyewe.

Mnapokea malipo kwa mikupuo?

Hapana, kwa sasa hatufanyi hivyo.

Taarifa za kadi yangu zitakuwa salama?

Unapofanya manunuzi kwenye mtandao tunachukua tahadhari kwa kutumia njia za usalama zilizo wazi kulinda taarifa za mtumiaji zilizo ndani ya uwezo wetu na kuzuia upatikanaji wa taarifa hizo kwa watu wengine. Tunachukua hatua mbalimbali za usalama kuhakikisha taarifa zako zinabaki kuwa salama pindi ufanyapo miamala nasi.

Hatua zetu za usalama

Bei Chee haitunzi taarifa binafsi za kadi zinazotumika kwa manunuzi. Malipo unayofanya kupitia tovuti yetu hufanyiwa kazi na wawakilishi wetu wenye sifa stahili.

Ulinzi gani unatolewa kwa wanunuzi wa Bei Chee?

Kama umelipia mtandaoni kabla ya kupokea bidhaa, basi Bei Chee itakulinda dhidi ya bidhaa ambayo haijafika, iliyoharibika, au ambayo inatofauti kabisa na uliyooda

Kiufundi

Nawezaje kufuta oda yangu?

Bofya kwenye menyu upande wa juu kulia kwenye ukurasa wa mwanzo wa Bei Chee. Bofya kundi unalokusudia kutafuta bidhaa kama vile laptop, TV nk. Kisha utapelekwa kwenye ukurasa wa kundi ulilochagua kutazama zaidi.

Nawezaje kufuta oda yangu?

Unaweza kutupigia simu kupitia namba 0762 493 434 au WhatsApp kupitia namba hiyo hiyo au tunadikie barua pepe [email protected] kwaajili ya kufuta oda ukiandika namba ya oda au ingia kwenye akaunti yajo na kisha bofya ‘Futa oda’. Ni rahisi.

Nawezaje kufuatilia oda yangu?

Utapokea barua pepe na ujumbe wa simu mara kwa mara kuhusu hali ya oda yako. Unaweza pia kuingia kwenye akaunti yako na kufuatilia hali halisi ya oda yako.

Urejeshaji

Kuna sera gani juu ya kurudisha bidhaa?

Bei Chee inayosera nzuri kabisa kuhusiana na urudishaji wa fedha na bidhaa.

Tafadhali bofya https://beichee.co.tz/utumaji-na-urejeshaji/?lang=sw kujua zaidi.

Nimepokea bidhaa mbovu?

Katika mazingira haya utahitaji kubadilishiwa bidhaa ama kurudishiwa fedhaa yako, chochote kati hayo itakachoonekana kinafaa zaidi kwako.

Naweza rudishiwa pesa zangu ata kama bidhaa haina mapungufu?

Mara nyingi hii haitawezekana. Bei Chee imeweka sera nzuri ya kurudhisha bidhaa na fedhaa. Tafadhali bofya https://beichee.co.tz/utumaji-na-urejeshaji/?lang=sw kujua zaidi.

Ntapokeaje fedha yangu nnayorudishiwa?

Taratibu za kukurudishia fedha zako huanza baada ya kuhakiki bidhaa uliyoirudisha. Tutakutumia barua pepe baada ya taratibu za kuhakiki bidhaa uliyoirudisha kukamilika. Zingatia, baadhi ya njia za kurudisha fedha zinajumuisha njia uliyotumia kulipia mara ya kwanza.

Itaachukua muda gani kukamilisha kurudishiwa fedha zangu?

Katika hali ya kawaida utapokea fedha zako ndani ya siku 7 baada ya kurudisha bidhaa yako. Fedha hurudishwa kwa njia ile ile uliyotumia kulipia.

All search results